
Yapi Malengo ya Shule yetu
Kujenga misingi bora kwa elimu bora ya mwanao na Taifa letu. Kufanikisha malengo haya shule imehakikisha yafuatayo kama baadhi ya mambo muhimu ;
- Somo la kompyuta na kompyuta za majaribio
- Maktaba ina vitabu vya kutosha vya kiada na ziada
- Bustani ya mbogamboga kwa chakula bora shuleni
- Mawasiliano bora ya wazazi wa wanafunzi kufuatilia
- Uhuru wa kuabudu kufuatana na dini ya mwanafunzi
- Bwalo na jiko la kisasa kwa mazingira na afya bora
- Ushirikiano mzuri wa jamii inayozunguka shule
- Uwepo wa maji ya kutosha kwa matumizi ya shule
- Shule ina uzio na ulinzi wa kutosha kwa ajili ya wanafunzi
- Tunafikika kwa barabara ya lami, mt. 600 toka barabara kuu
- Shule ni ya kutwa na bweni kwa wasichana na wavulana
- Usafiri unapatikana kwa wanafunzi wa kutwa
Faida za kumleta mwanao kujiunga
St. Anne Pre & Primary School
Hii ni shule ya muda mrefu na yenye waalimu wazoefu na wa kiwango kikubwa cha taalum zao kumfanya mwanao kufaulu vyema kwenye masomo yake